12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani. 13 Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imeniwia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Eze 9:4,6BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
16 2 Fal 13:23;24:20;Yer 23:39;52:3Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, Mashariki mwa Edeni.