3 Kum 21:17Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,
Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.
Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
4 Kum 27:20;1 Nya 5:1Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena,
Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako,
Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.