9 Hes 24:9Yuda ni mwanasimba,
Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;
Aliinama akajilaza kama simba,
Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?
10 Hes 24:17;Zab 60:7;1 Nya 5:2;Isa 11:1;Eze 21:27;Dan 9:25;Mt 21:9;Lk 1:32;Isa 2:2;11:10;60:1-5;Hag 2:7;Lk 2:30;2 Fal 18:32Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,
Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,
Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,
Ambaye mataifa watamtii.