Uovu wa wanadamu
1 Ayu 1:6;2:1Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 2 Kor 6:18;Kum 7:3,4wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua. 3 Lk 19:42;Gal 5:16,17;1 Pet 3:20;Zab 78:39BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini. 4 Hes 13:33Nao Wanefili6:4 Wanefili: maana yake ni majitu. walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. 5 Rum 1:28-31;Mwa 8:21;Kum 29:19;Mit 6:18;Mt 15:19;Mt 24:37;Lk 17:26;1 Pet 3:20BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 6 Hes 23:19;1 Sam 15:11,29;Isa 63:10;Efe 4:30BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba. 8 Mwa 19:19;Kut 33:12;Lk 1:30;Mdo 7:46Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Nuhu atengeneza safina
9 2 Pet 2:5Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.