5 Rum 1:28-31;Mwa 8:21;Kum 29:19;Mit 6:18;Mt 15:19;Mt 24:37;Lk 17:26;1 Pet 3:20BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 6 Hes 23:19;1 Sam 15:11,29;Isa 63:10;Efe 4:30BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba. 8 Mwa 19:19;Kut 33:12;Lk 1:30;Mdo 7:46Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Nuhu atengeneza safina
9 2 Pet 2:5Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.