Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 9:12-17

SRUV Swahili Revised Union Version

12 Mt 26:26-28Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; 13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. 14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, 15 Kut 28:12;Law 26:42,45;Eze 16:60;Isa 54:9nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. 16 Mwa 17:13,19;2 Sam 23:5Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. 17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na watu wote walioko katika nchi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Mungu akasema, "Hii ni ishara ya agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, agano kwa vizazi vyote vijavyo: 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia. 14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukatokea mawinguni, 15 nitakumbuka agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. 16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani."

    17 Hivyo Mungu akamwambia Nuhu, "Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 Mungu akasema, "Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo: 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. 14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni, 15 nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. 16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani."

    17 Hivyo Mungu akamwambia Noa, "Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.