Publicidade

Joel 1

Maombolezo juu ya maangamizi ya nchi

1 Ebr 1:1;2 Pet 1:21 Neno la BWANA lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.

2 Kum 4:32;Isa 7:17;Dan 12:1;Yoe 2:2;Mt 24:21 Sikieni haya, enyi wazee;

Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi.

Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu,

Au katika siku za baba zenu?

3 Zab 78:4 Waambieni watoto wenu habari yake,

Watoto wenu wakawaambie watoto wao,

Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.

4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.

5 Isa 32:10 Levukeni, enyi walevi, mkalie;

Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;

Kwa sababu ya divai mpya;

Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.

6 Mit 30:25;Ufu 9:8 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,

Lenye nguvu, tena halina hesabu;

Meno yake ni kama meno ya simba,

Naye ana magego ya simba mkubwa.

7 Isa 5:6 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.

8 Isa 22:12;Mit 2:17 Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia

Kwa ajili ya mume wa ujana wake.

9 Yoe 2:14 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji

Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;

Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

10 Yer 12:11;Isa 24:7 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.

11 Yer 14:3 Tahayarini, enyi wakulima;

Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;

Kwa ajili ya ngano na shayiri,

Maana mavuno ya mashamba yamepotea.

12 Isa 9:3;Yer 48:33;Hos 9:1,2 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;

Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;

Naam, miti yote ya mashamba imekauka;

Maana furaha imetoweka kwa wanadamu.

Mwito wa toba na sala

13 Yer 4:8 Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;

Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;

Njooni mlale usiku kucha katika magunia,

Enyi wahudumu wa Mungu wangu;

Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji

Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.

14 2 Nya 20:3,13 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,

Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;

Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,

Na kumlilia BWANA,

15 Yer 30:7;Yoe 2:3;Amo 5:16-18;Isa 13:6 Ole wake siku hii!

Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi. 16 Kum 12:7,12;16:11 Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu? 17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; mabohari yameachwa ukiwa; ghala zimeharibika; kwa maana nafaka imekauka. 18 1 Fal 18:5;Hos 4:3 Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.

19 Ee BWANA, nakulilia wewe;

Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,

Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.

20 Ayu 38:41;Zab 104:31;1 Fal 17:7 Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe;

Kwa maana vijito vya maji vimekauka,

Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.

Veja também

Joel
Ver todos os capítulos de Joel
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-