Roho wa Mungu amiminiwa
28 Isa 44:3;Yn 7:39;Isa 54:13;Mdo 2:17-21;21:9Hata2:28 Katika Kiebrania ni Sura 3:1. itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 1 Kor 12:13;Gal 3:28tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30 Mk 13:24Nami nitaonesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. 31 Mt 24:29;Mk 13:24-25;Lk 21:25;Ufu 6:12-13Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo. 32 Zab 50:15;Yer 33:3;Mdo 2:21;1 Kor 1:2;Isa 46:13;11:11;Oba 1:17;Rum 10:13;9:27Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.