13 Yn 15:7;Mk 11:24;1 Yoh 5:14Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14 Yn 16:23,24Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
15 Yn 15:10;1 Yoh 5:3Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16 Yn 14:26;15:26;16:7;1 Yoh 2:1Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;