1 Yn 14:27;Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Yn 12:26;17:24 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia. 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? 6 Ebr 10:20;Mt 11:27;Yn 11:25;Rum 5:1,2 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8 Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. 9 Yn 12:45;Ebr 1:3;Mt 17:17 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? 10 Yn 12:49 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11 Yn 14:20;Yn 10:25,38 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12 Mk 16:19,20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13 Yn 15:7;Mk 11:24;1 Yoh 5:14 Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14 Yn 16:23,24 Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
15 Yn 15:10;1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16 Yn 14:26;15:26;16:7;1 Yoh 2:1 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 Yn 7:39;16:13;Mt 10:20;Rum 8:26 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19 Yn 16:16 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Yn 17:21-23 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21 2 Kor 3:18;1 Yoh 5:3 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22 Mdo 10:41 Yuda (siye Iskarioti), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23 Yn 13:34;14:21;Mit 8:17;Mt 18:20;28:20;Efe 3:17;2 Kor 6:16 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Yn 7:16;1 Yoh 2:5 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma.
25 Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26 Yn 14:16;Mt 10:19 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Yn 1:16,33;Flp 4:7 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28 Yn 14:3,6,18;Lk 24:52 Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Yn 13:19 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, ili litakapotokea mpate kuamini. 30 Yn 12:31;Efe 2:2 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31 Yn 10:18;Mt 26:46;Mk 14:42 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.