Publicidade

João 17

Yesu awaombea wanafunzi wake

1 Yn 11:14;13:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2 Mt 11:27 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya watu wote,17:2 au wote wenye mwili. ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3 1 Yoh 5:20;1 The 1:9 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Yn 4:34 Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 5 Yn 1:1;17:24;Flp 2:6 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 6 Yn 17:9;Mt 6:9 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8 Yn 16:30 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nilitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 9 Yn 6:37,44 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 10 Yn 16:15;Lk 15:31 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

11 Yn 10:30;Mt 6:13 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12 Zab 41:9;109:8;Yn 13:18;6:39;2 The 2:3 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13 Yn 15:11 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14 Yn 15:19 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 2 The 3:3;1 Yoh 5:18;Mt 6:13;Lk 22:32 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17 Yn 6:63 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18 Yn 20:21 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo niliwatuma hao ulimwenguni. 19 Ebr 10:10 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

20 Yn 17:9 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Gal 3:28 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Mdo 4:32 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 1 Kor 6:17;Gal 2:20 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24 Yn 10:29;12:26;Efe 1:4 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nilikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami niliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-