Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 18:12,13,19,24

SRUV Swahili Revised Union Version

Yesu mbele ya kuhani mkuu

12 Mt 26:57-75;Mk 14:53-72;Lk 22:54-71Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga. 13 Wakampeleka kwa Anasi kwanza; maana alikuwa baba mkwe wa Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule.

Kuhani Mkuu amhoji Yesu

19 Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake, na kuhusu mafundisho yake. 24 Basi Anasi akampeleka akiwa amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Hivyo wale askari, wakiwa na jemadari wao na maafisa wa Wayahudi, wakamkamata Isa na kumfunga. 13 Kwanza wakampeleka kwa Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule.

    19 Wakati huo kuhani mkuu akawa anamuuliza Isa kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake.

    24 Ndipo Anasi akampeleka Isa kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 Hivyo wale askari, wakiwa pamoja na majemadari wao na maafisa wa Wayahudi, wakamkamata Yesu na kumfunga. 13 Kwanza wakampeleka kwa Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule.

    19 Wakati huo kuhani mkuu akawa anamuuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake.

    24 Ndipo Anasi akampeleka Yesu kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.