19 Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. 20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kigiriki.
Publicidade
Yohana 19:19,20
SRUV Swahili Revised Union Version
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
19 Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Isa; likasema:
Isa Al-Nasiri
Mfalme wa Wayahudi.
20 Kwa kuwa mahali hapo Isa aliposulubiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
19 Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu, likasema: "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi." 20 Kwa kuwa mahali hapo Yesu aliposulubiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.