Yesu awatokea wanafunzi
19 Mk 16:14-18;Lk 24:36-49Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. 20 1 Yoh 1:1Naye akiisha kusema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. 21 Yn 17:18Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi. 22 Mwa 2:7Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mt 16:19;18:18Na wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.