Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 21:9,15-19

SRUV Swahili Revised Union Version

9 Basi waliposhuka pwani, wakaona huko moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate.

15 Yn 1:42Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda21:15 Katika lugha ya Kigiriki neno hili kupenda lina maana mbili. Maana yake ya pili husomeka hivi, 15 Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa ni rafiki yako. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. 16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa ni rafiki yako. Akamwambia, Chunga kondoo wangu. 17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, u rafiki yangu? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, U rafiki yangu? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua yakuwa ni rafiki yako. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu. kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. 16 1 Pet 5:2,4Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo wangu. 17 Yn 13:38;16:30Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.

18 Mt 16:22;26:39Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka. 19 Yn 13:36Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.

    15 Walipokwisha kula, Isa akamuuliza Simoni Petro, "Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?"

    Yeye akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."

    Isa akamwambia, "Lisha wana-kondoo wangu."

    16 Isa akamuuliza tena, "Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?"

    Petro akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."

    Isa akamwambia, "Chunga kondoo wangu."

    17 Kwa mara ya tatu Isa akamuuliza Petro, "Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?"

    Petro akahuzunika sana kwa kuwa Isa alimuuliza mara ya tatu, "Unanipenda?" Akamjibu, "Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda."

    Isa akamwambia, "Lisha kondoo wangu. 18 Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka. Lakini utakapokuwa mzee, utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda." 19 Isa alisema haya ili kuashiria aina ya kifo ambacho Petro angemtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, "Nifuate!"

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    9 Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.

    15 Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, "Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?"

    Yeye akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."

    Yesu akamwambia, "Lisha wana-kondoo wangu."

    16 Yesu akamwambia tena, "Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?"

    Petro akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."

    Yesu akamwambia, "Chunga kondoo zangu."

    17 Kwa mara ya tatu Yesu akamuuliza Petro, "Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?"

    Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimuuliza mara ya tatu, "Unanipenda?" Akamjibu, "Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda."

    Yesu akamwambia, "Lisha kondoo wangu. 18 Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda." 19 Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, "Nifuate!"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.