Yesu aponya katika siku ya sabato
1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.
2 Na huko Yerusalemu karibu na mlango wa kondoo pana bwawa la maji liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha, nalo lilikuwa na matao matano. 3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. 4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika lile bwawa, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] 5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa mgonjwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa katika hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? 7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia katika bwawa, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. 8 Mt 9:6Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. 9 Yn 9:14Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.