21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao. 22 Dan 7:13,14;Mdo 17:31Tena Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote; 23 Flp 2:10,11;1 Yoh 2:23;Lk 10:16ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyemtuma. 24 Yn 3:16,18;8:51;1 Yoh 3:14Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ana uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. 25 Mt 8:22;Efe 2:5,6Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Yn 1:1-4Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. 27 Dan 7:10,14;Yn 5:22Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa inakuja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Dan 12:2;Yn 6:40;Mt 16:27Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
30 Yn 5:19;6:38Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenituma. 31 Yn 8:14Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.