44 Yn 6:55Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Isa 54:13;Yer 31:33,34Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu. 46 Yn 1:18Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. 47 Yn 3:16Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye anao uzima wa milele.