Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 9

Mtu aliyezaliwa kipofu apata kuona

1 Mdo 3:2;14:8Na alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Lk 13:2;Kut 20:5Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 3 Yn 11:4Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 4 Yn 5:17,20;11:9Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 5 Mt 5:14;Yn 8:12;12:35Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 6 Mk 8:23Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni, 7 akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona. 8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? 9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? 11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona. 12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.

Veja também