Mtu aliyezaliwa kipofu apata kuona
1 Mdo 3:2;14:8Na alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Lk 13:2;Kut 20:5Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 3 Yn 11:4Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 4 Yn 5:17,20;11:9Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 5 Mt 5:14;Yn 8:12;12:35Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 6 Mk 8:23Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni, 7 akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona.