Publicidade

Josué 3

14 Kut 25:10;26:30;Hes 10:3;2 Nya 6:41;Zab 132:8;Mdo 7:45;Ebr 9:4Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la Agano wakatangulia mbele ya watu, 15 1 Nya 12:15;Yer 12:5;49:19;Yos 4:18;5:10,12basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), 16 1 Fal 4:12;7:46;Kum 3:17;Mwa 14:3;Hes 34:3ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa kichuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyoteremkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yataacha kutiririka kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. 17 Kut 14:29;Ebr 11:29Na hao makuhani waliolichukua sanduku la Agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hadi taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-