Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 4:4-9

SRUV Swahili Revised Union Version

4 2 Fal 22:14;1 Kor 1:27Basi Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. 5 Mwa 35:8Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue. 6 Ebr 11:32;Yos 19:37Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: "Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori". 7 Kut 14:4;Yos 11:20;Eze 38:10-16;Yoe 3:11-14;Amu 5:21;1 Fal 18:40;Zab 83:9Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako. 8 Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. 9 Amu 2:14;3:8;Zab 44:12;Isa 50:1Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    4 Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye alikuwa anaamua Israeli wakati ule. 5 Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue. 6 Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, "Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume elfu kumi toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori. 7 Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake ya vita na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ "

    8 Baraka akamwambia, "Ukienda pamoja nami nitaenda, lakini usipoenda pamoja nami, sitaenda."

    9 Debora akamwambia, "Hakika nitaenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Mwenyezi Mungu atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke." Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka hadi Kedeshi,

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    4 Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye alikuwa anaamua Israeli wakati ule. 5 Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue. 6 Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, "Bwana, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori. 7 Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ "

    8 Baraka akamwambia, "Ukienda pamoja nami nitakwenda, lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda."

    9 Debora akamwambia, "Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Bwana atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke." Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi,

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.