Unabii wa Zekaria
67 Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,
68 Lk 7:16;Zab 41:13;72:18Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,
Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.
69 1 Sam 2:10;Zab 18:2;132:17Ametusimamishia pembe ya wokovu
Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
70 Kama alivyosema tangu mwanzo
Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu;
71 Zab 106:10Tuokolewe na adui zetu
Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
72 Zab 105:8;106:45;Mwa 17:7;Law 26:42Ili kuwatendea rehema baba zetu,
Na kulikumbuka agano lake takatifu;
73 Mwa 22:16,17;Mik 7:20Kiapo alichomwapia Abrahamu, baba yetu,
74 Tit 2:12,14Ya kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke mikononi mwa adui zetu,
Na kumwabudu pasipo hofu,
75 Kwa utakatifu na kwa haki
Mbele zake siku zetu zote.
76 Mal 3:1;Mt 3:3Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye Juu,
Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake;
77 Yer 31:34Uwajulishe watu wake wokovu,
Kwa kusamehewa dhambi zao.
78 Hes 24:17;Isa 60:1,2;Mal 4:2Kwa njia ya rehema za Mungu wetu,
Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,
79 Isa 9:2;58:8;Mt 4:16Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti,
Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.