Mfano wa Msamaria mwema
25 Mt 22:35-40;Mk 12:28-34Na tazama, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?Lk 18:18-2026 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27 Law 19:18;Kum 6:5Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28 Law 18:5;Mt 19:17Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.