Kuomba bila kukoma
5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, 6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; 7 Mt 26:10na yule wa ndani amjibu akisema, Usinisumbue; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kutoka nikupe? 8 Lk 18:5Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa hatoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, atatoka na kumpa kadiri ya haja yake.