Yesu amponya mtu mwenye ugonjwa wa safura
1 Lk 6:6-11;11:37Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. 2 Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura. 3 Yesu akajibu, akawaambia wanasheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? 4 Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake.