Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 17

Yesu awaponya watu kumi wenye ukoma

11 Lk 9:51;13:22Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. 12 Law 13:45,46Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, 13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! 14 Law 13:49;14:1-32;Lk 5:14Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. 15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; 16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. 17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi? 18 Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? 19 Lk 7:50Akamwambia, Inuka, nenda zako, imani yako imekuokoa.

Veja também