Yesu amponya mwombaji kipofu
35 Mt 20:29-34;Mk 10:46-52Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka; 36 na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini? 37 Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita. 38 Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu. 39 Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu. 40 Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza, 41 Unataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona. 42 Lk 17:19Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya. 43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.