Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 19

Yesu na Zakayo

1 Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. 2 Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. 3 Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. 4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. 5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Lk 15:2Hata watu walipoona, walinung’unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. 8 Kut 22:1;Hes 5:6,7Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. 9 Lk 13:16;Mdo 3:25;16:31Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu. 10 Mt 18:11;Eze 34:16;Yn 3:17;Lk 5:32;1 Tim 1:15Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Veja também