Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 2

25 Isa 40:1;49:13Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29 Mwa 46:30Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako,

Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Isa 40:5;52:10Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Isa 42:6;49:6;52:10Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa,

Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

Veja também