Kuja kwa Mwana wa Adamu
25 Mt 24:29,30;Mk 13:24-26Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa kuvuma kwa habari na mawimbi yake; Isa 13:10;Eze 32:7;Yoe 2:31;Ufu 6:12-13;Zab 65:726 Isa 34:4watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. 27 Dan 7:13;Ufu 1:7;Mt 26:64Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 28 Flp 4:4,5Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.