Mahimizo ya kuwa waangalifu
34 Lk 17:27;Mk 4:19;Mt 24:49Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo; 35 Isa 24:17;1 The 5:3kwa kuwa ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. 36 Mk 13:33;Ufu 6:17Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.