Kusalitiwa na kukamatwa kwa Yesu
47 Mt 26:47-56;Mk 14:43-49;Yn 18:2-11Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. 48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?