Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 24:13,15,16,30-32

SRUV Swahili Revised Union Version

Matembezi ya kwenda Emau

13 Mk 16:12,13Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda katika kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. 15 Mt 18:20Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. 16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue. 30 Lk 22:19Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. 31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia Maandiko?

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    13 Ikawa siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Isa walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba24:13 kama kilomita 11 kutoka Yerusalemu. 15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Isa mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 16 lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.

    30 Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. 32 Wakaulizana wao kwa wao, "Je, mioyo yetu haikuwaka ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?"

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    13 Ikawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba24:13 Maili saba ni kama kilomita 11.2. kutoka Yerusalemu. 15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 16 lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.

    30 Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. 32 Wakaulizana wao kwa wao, "Je, mioyo yetu haikuwakawaka kwa furaha ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.