Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 24:39-43

SRUV Swahili Revised Union Version

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. 40 Na baada ya kusema hayo aliwaonesha mikono yake na miguu yake. 41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula chochote hapa? 42 Yn 21:5,10Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. 43 Akakitwaa, akala mbele yao.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi mwenyewe. Niguseni mwone; kwa maana mzuka huna nyama na mifupa, kama mnavyoniona mimi."

    40 Aliposema haya, akawaonesha mikono na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, "Mna chakula chochote hapa?"

    42 Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 43 naye akakichukua na kukila mbele yao.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo."

    40 Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, "Mna chakula chochote hapa?"

    42 Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 43 naye akakichukua na kukila mbele yao.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.