Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 3:10-14

SRUV Swahili Revised Union Version

10 Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? 11 Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. 12 Lk 7:29Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi? 13 Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. 14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    10 Umati ule wa watu wakamuuliza, "Inatupasa tufanyeje basi?"

    11 Yahya akawaambia, "Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo."

    12 Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, "Mwalimu na sisi inatupasa tufanyeje?"

    13 Akawaambia, "Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa."

    14 Askari nao wakamuuliza, "Je, nasi inatupasa tufanye nini?"

    Akawaambia, "Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    10 Ule umati wa watu ukamuuliza, "Inatupasa tufanyeje basi?"

    11 Yohana akawaambia, "Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo."

    12 Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, "Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?"

    13 Akawaambia, "Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa."

    14 Askari nao wakamuuliza, "Je, nasi inatupasa tufanye nini?"

    Akawaambia, "Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.