Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 5

Yesu awaita wanafunzi wa kwanza

1 Mt 13:1-2;Mk 3:9-10;4:1Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti, 2 akaona mashua mbili zimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia katika mashua moja, ndiyo yake Simoni, akamtaka aipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano akiwa katika mashua. 4 Yn 21:6Na alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5 Yn 21:3Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6 Yn 21:6Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; 7 wakawapungia mikono washiriki wenzao waliokuwa katika mashua nyingine, waje kuwasaidia; wakaja, wakazijaza mashua zote mbili, hata zikakaribia kuzama. 8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini mbele ya Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 9 Maana alishikwa na mshangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki waliowapata; 10 Mt 13:47na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. 11 Mt 19:27Hata walipokwisha kuziegesha mashua zao pwani, wakaacha vyote wakamfuata.

Veja também