Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 6

Mtu mwenye mkono uliopooza

6 Mt 12:9-14;Mk 3:1-6Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kulia umepooza. 7 Lk 14:1Na Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kama ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia. 8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama. 9 Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? 10 Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

Veja também