Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 7

Yesu amfufua mtoto wa mama mjane

11 Baadaye kidogo alikwenda mpaka katika mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. 12 Lk 8:42;1 Fal 17:17Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wengi mjini walikuwa pamoja naye. 13 Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15 1 Fal 17:23;2 Fal 4:36Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16 Lk 1:68;19:44Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. 17 Habari hii yake ikaenea kote katika Yudea yote, na katika nchi zote za karibu.

Veja também