Baadhi ya wanawake waandamana na Yesu
1 Lk 4:43Ikawa baada ya hayo alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza Habari Njema ya ufalme wa Mungu; na wale Kumi na Wawili walikuwa pamoja naye, 2 Mt 27:55-56;Mk 15:40-41;16:9;Lk 23:49na wanawake kadhaa ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.