Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 8

22 Mt 8:18,23-27;Mk 4:35-41Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. 23 Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, mashua ikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. 24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. 25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também