Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 9

27 Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu.

Kugeuka sura

28 2 Pet 1:17-18;Mt 17:1-9;Mk 9:2-9Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba. 29 Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. 30 Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; 31 Lk 9:22walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu.

Veja também