Yesu awaponya wengi katika nyumba ya Simoni
29 Mt 8:14-16;Lk 4:38-41Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. 30 Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, akiugua homa; na mara wakamwambia habari zake. 31 Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.