Yesu amtakasa mtu mwenye ukoma
40 Mt 8:2-4;Lk 5:12-16Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. 41 Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. 42 Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.