23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! 24 Zab 62:10;1 Tim 6:17Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! 25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26 Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka? 27 Mwa 18:14;Ayu 42:2Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu.
Marko 10:23-27
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
23 Isa akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!"
24 Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, "Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika ufalme wa Mungu. 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
26 Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, "Ni nani basi awezaye kuokoka?"
27 Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
23 Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika Ufalme wa Mungu!"
24 Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, "Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu. 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri10:25 Tajiri ina maana wale wanaotumainia mali. kuingia katika Ufalme wa Mungu."
26 Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, "Ni nani basi awezaye kuokoka?"
27 Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.