Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 11

Yesu aingia Yerusalemu kwa shangwe

1 Mt 21:1-9;Lk 19:29-38;Yn 12:12-16Walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake, 2 akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwanapunda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. 3 Mk 14:14Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa. 4 Wakaenda zao, wakamwona mwanapunda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. 5 Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwanapunda? 6 Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza, nao wakawaruhusu. 7 Wakamletea Yesu yule mwanapunda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake. 8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani. 9 Zab 118:25-26Nao watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana; 10 umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni.

11 Mt 21:12-22;Lk 19:45-48Naye akaingia Yerusalemu hata ndani ya hekalu; na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka, akaenda Bethania pamoja na wale Kumi na Wawili.

Veja também