Yesu aulaani mtini
12 Siku iliyofuata walipokuwa wakitoka Bethania, aliona njaa. 13 Lk 3:9;13:6-9Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. 14 Mk 11:20Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.