Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 11

Fundisho kutoka kwa mtini ulionyauka

20 Mk 11:14Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. 21 Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. 22 Yn 14:1Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. 23 Mt 17:20;1 Kor 13:2;Lk 17:6Amin, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. 24 Mt 7:7;Yn 14:13;16:23Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. 25 Mt 5:23;6:14-15Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [

Veja também