Kuja kwa Mwana wa Adamu
24 Isa 13:10;Eze 32:7;Yoe 2:10,31;3:15;Ufu 6:12Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. 25 Isa 34:4;Yoe 2:10;Mdo 6:13Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. 26 Dan 7:13;Ufu 1:7Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. 27 Zek 2:6;Kum 30:4;Mt 13:41Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.