34 Yn 12:27;Zab 43:5Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe. 35 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana, saa hiyo imwepuke. 36 Mk 10:38Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; lakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.
Marko 14:34-36
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
34 Akawaambia, "Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe."
35 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. 36 Akasema, "Abba14:36 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba., Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
34 Akawaambia, "Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe."
35 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. 36 Akasema, "Abba,14:36 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; ni mtoto wa kuzaa tu angeweza kulitumia kwa baba yake. Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.